close
Nenda kwa yaliyomo

Venezuela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
República Bolivariana de Venezuela1
Jamhuri ya Kibolivar ya Venezuela1
Bendera ya Venezuela Nembo ya Venezuela
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: None 2
Wimbo wa taifa: Gloria al Bravo Pueblo
Lokeshen ya Venezuela
Mji mkuu Caracas
10°30 N 66°58 W
Mji mkubwa nchini Caracas
Lugha rasmi Kihispania 3
Serikali Shirikisho la jamhuri
Delcy Rodriguez (Kaimu)
Uhuru
Kutoka Hispania
Kutoka Gran Colombia
ilitambuliwa

5 Julai 1811
21 Novemba 1831
30 Machi 1845
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
916,445 km² (ya 32)
3.2
Idadi ya watu
 - 2024 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
28,517,000 (ya 53)
23,054,210
30.2/km² (ya 175)
Fedha Bolivar (VEB)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
AST (UTC-4)
None (UTC)
Intaneti TLD .ve
Kodi ya simu +58

-

1 Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela imekuwa jina la nchi tangu katiba ya 1999. "Kibolivar" ni jina la heshima kwa kumbukumbu ya mshujaa wa uhuru Simon Bolivar.
2 Zamani: Dios y Federación ("Mungu na Shirikisho")
3 Katiba inatambua pia lugha asilia zote nchini.


Image
Ramani ya Venezuela.

Venezuela ni nchi iliyopo pwani ya kaskazini mwa Amerika ya Kusini. Jina lake rasmi ni Jamhuri ya Kibolivar ya Venezuela (Kihispania: República Bolivariana de Venezuela). Sehemu kubwa ya ardhi yake ipo barani, ingawa nchi ina visiwa mbalimbali katika Bahari ya Karibi. Venezuela ina eneo la kilomita za mraba 912,050 (maili za mraba 352,140). Idadi ya wakazi ni kati ya milioni 32 na milioni 28.[1][2][3] Utambuji wa takwimu maalumu unategemea shirika linalofanya makadirio. Idadi ya watu imepanda na kupunguka miaka iliyopita kama matokeo ya mgogoro wa kiuchumi uliotukia kuanzia mwaka 2010.

Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia barani. Nchi ipo pwani pa Bahari ya Karibi na Bahari ya Atlantiki. Mbele ya pwani ya Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.

Ndani ya nchi kuna majimbo ishirini na tatu, wilaya ya mji mkuu wa Caracas, na maeneo tegemezi ya baharini. Caracas ni mji mkubwa wa kwanza. Mji wa pili kwa ukubwa ni Maracaibo.[4][5] Wavenezuela wengi wanaishi pwani ya kaskazini, hasa karibu na Caracas. Venezuela ni mojawapo kati ya nchi zinazokuwa na mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu wanaosakini mijini.[4][5]

Venezuela ilikuwa koloni la Hispania kutoka mwaka 1522 hadi mwaka 1811. Upinzani wa wakazi wa asili ulikuwa kali. Wengi wao walitiwa utumwani kutoka mwanzo wa ukoloni, kama hawakuuawa. Halafu Venezuela ilikuwa mojawapo kati ya makoloni ya kwanza ya Hispania katika Amerika kutangaza uhuru wake karne ya 19. Ilikuwa sehemu ya Jamhuri ya Shirikisho la Kwanza la Kolombia (Kihispania: Gran Colombia). Ilitengeka kama dola huru mwaka 1830. Baadaye, karne ya 19, Venezuela ilipitia msukosuko wa kisiasa na utawala wa mabavu. Madikteta wa kieneo walitawala nchi hadi katikati ya karne ya 20. Kuanzia mwaka 1958, serikali mbalimbali za kidemokrasia zilitawala. Kwa kipindi hicho, nchi ilipitia ustawi wa kiuchumi.

Migogoro ya kifedha kadhaa miaka ya 1980 na 1990 ilisababisha migogoro ya kisiasa na msukosuko ya kijamii uliovuka nchi yote. Miongoni mwa matukio ya kipindi hicho kulikuwa na ghasia za Caracazo mwaka 1989, mapinduzi mawili mwaka 1992, na shtaka la Rais aliyebadhiria mifuko ya serikali mwaka 1993. Mwaka huo kesho, kwa sababu wananchi walipoteza imani kwa vyama vya kidesturi, uchaguzi wa 1998 ulileta ushindi wa Hugo Chávez na Mapinduzi ya Kibolivar. Mwanzo wa mapinduzi hayo ulikuwa Mkutano wa Katiba wa mwaka 1999.[6] Ongezeko la bei ya mafuta ya petroli liliziunga mkono sera za kiuchumi zilizozingatia manufaa ya umma.[7] Tukio hilo liliruhusu maongezeko ya uwekezaji kwa huduma kwa jamii na upungufu wa tofauti ya utajiri na umaskini miaka ya mapema ya serikali hiyo.[8][9][10][11] Kwa hali yoyote, umaskini ulipanda tena kwa kasi miaka ya 2010.[12][13] Unyofu wa matokeo ya chaguzi za miaka 2013, 2018, na 2024 zilishukiwa ndani na nje ya nchi.[14][15] Wagombea wa upinzani walishikwa au walifukuzwa. Maandamano makubwa yalijiri kama matokeo, vilevile shutuma ya madola mengi. Migogoro mingine ilianza kama matokeo.[16] Mwaka 2026 mwezi wa kwanza tarehe 4, Marekani iliteka Rais wa Venezuela Nicolás Maduro. Nchi hiyo ilitangaza kuwa ingeiongoza Venezuela hadi serikali ya kitambo ingeweza kuundwa.[17] Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa nchi yake ingedhibiti kuuza nje kwa mafuta ya petroli ya Venezuela.[18]

Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri ya kirais. Kwa hali yoyote, nchi ilikengeua kuwa mabavu zaidi tangu mwanzo wa utawala wa Hugo Chávez na Nicolás Maduro.[19] Nchi iko mahali kubaya orodhani kwa uhuru wa magazeti, haki za raia, na usimamizi wa ufisadi. Hakuna uhuru wa kimahakama.[20] Ni nchi inayoendelea, na ina hazina kubwa zaidi za mafuta za dunia.[21] Mara moja, Venezuela ilikuwa nchi isiyoendelea iliyokuwa hasa muuzaji wa bidhaa za kilimo kama buni na kokwa za kakao. Hata hivyo, mafuta yalishinda haraka kuwa bidhaa nje kuu ya nchi na chanzo kikuu cha mapato ya serikali. Miongoni mwa shida za nchi ni mfumko wa bei kali,[22][23] uhaba wa bidhaa za haja,[24][25][26] ukosefu wa ajira,[27] umaskini unaoenea pote,[28] ugonjwa, kiwango cha vifo vya watoto wachanga kikubwa, utapiamlo, changamoto za mazingira, matatizo ya uhalifu makali, na ufisadi mkali. Vikwazo vya mali ya nje vilivyowekwa na Marekani viligharimu nchi kati ya dola ya Marekani bilioni 24 na 30.[29] Hali hizi zimechangia tatizo la wakimbizi wakati ambapo kati ya watu milioni 6.8 na milioni 7.9 wameondoka nchi hadi Mei 2025.[3][30][31] Hadi mwaka 2017, Venezuela imetangazwa kukosekana kuhusu malipo yake mashirika ya makadirio ya mkopo.[32][33] Migogoro hii imekuwa sababu kuu ya uvunjaji wa haki za binadamu uozidishika.

Lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa ya Venezuela.

Asili ya jina "Venezuela"

[hariri | hariri chanzo]
Image
Nyumba ya "palafito" jinsi ilivyoonekana zamani za Amerigo Vespucci.

Jina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Amerigo Vespucci, mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania, aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katikati ya maji karibu na mwambao pasipo kina. Vijiji vilimkubusha mji wa Venezia uliojengwa vilevile. Venezuela yamaanisha "Venezia Ndogo" katika Kihispania.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Venezuela ipo kaskazini mwa Amerika ya Kusini inayofanya sehemu ya bamba la Amerika ya Kusini kuhusu gandunia. Ni nchi ya 32 kwa ukubwa, ikiwa na eneo la jumla la km² 916,445 (kama Namibia), ikiwa na kipimo cha eneo ardhini cha km² 882,050. Maeneo ya Venezuela yapo baina ya ikweta na latitudo 16°N (kaskazini), na baina ya longitudo 59° na 74°W (magharibi).

Venezuela inaonekana kuwa na umbo wa pembetatu, ikiwa na pwani yenye urefu wa km 2,800 (mi 1,700). Miongoni mwapwani hizi ni visiwa vingi katika Bahari ya Karibi na sehemu fupi iliyopakana Bahari ya Atlantiki kaskazini. Kuna kanda nne za kijiografia thabiti:

  • Tambarare za pwani karibu na Maracaibo katika kaskazini-magharibi
  • Milima ya Andes katika kaskazini-magharibi ikiyoshika eneo kubwa kuenea magamaga pwani ya Karibi kwa kiasi kikubwa kutoka magharibi mpakani pa Kolombia mpaka mashariki katika pwani kaskazini.
  • Tambarare pana za mto Orinoco katikati ya nchi.
  • Nyanda za juu za Guyana katika kusini-mashariki.

Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kilimo ni 4%, eneo la mifugo 20%, na mazao ya kudumu kama kahawa 1%.

Milima ya meza

[hariri | hariri chanzo]
Image
Mlima wa meza Mt. Roraima

Nyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee: kuna milima ya meza 115 inayoitwa "tepui" katika lugha ya wakazi asilia. Kiekolojia hilo ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama wa pekee, tofauti na milima jirani, na inapatikana hapa tu kote duniani. Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko ya Salto del Angel ("anguko la malaika") ambako maji huanguka mita 965.

Mto mkubwa wa Venezuela ni Orinoco wenye urefu wa km 2574 unaoishia katika Atlantiki. Lakini mkono wa Brazo Casiquiare unajitenga na kuishia katika mto wa Amazonas nchini Brazil. Matawimto muhimu ya Orinoco ni Rio Apure na Rio Caroni.

Majimbo katika shirikisho

[hariri | hariri chanzo]
Image
Los Barrios ni mitaa ya vibanda vya Caracas

Venezuela ni shirikisho la majimbo 23 ya kujitawala, maeneo yasiyojitawala na eneo la shirikisho la Caracas.

Jimbo Mji Mkuu Wakazi Eneo Kanda
AmazonasPuerto Ayacucho70,464180,144 km²Guayana
AnzoáteguiBarcelona1,222,22543,300 km²Nor - Oriental
ApureSan Fernando de Apure377,75676,500 km²Llanos
AraguaMaracay1,449,6167,014 km²Central
BarinasBarinas624,50835,200 km²Andean
BolívarCiudad Bolívar1,214,846238.000 km²Guayana
CaraboboValencia1,932,1684,650 km²Central
CojedesSan Carlos253,10514,800 km²Central
Delta AmacuroTucupita97,98740,200 km²Guayana
FalcónCoro763,18024,800 km²Central - Occidental
GuáricoSan Juan de los Morros627,08664,986 km²Llanos
LaraBarquisimeto1,556,41519,800 km²Central - Occidental
MéridaMérida715,26811,300 km²Andean
MirandaLos Teques2,330,8727,950 km²Capital
MonagasMaturín712,62628,930 km²Nor - OrientalImage
Nueva EspartaLa Asunción712,6261,150 km²InsularImage
PortuguesaGuanare725,74015,200 km²Central - Occidental
SucreCumaná786,48311,800 km²Nor - Oriental
TáchiraSan Cristóbal992,66911,100 km²South - Occidental
TrujilloTrujillo608,5637,400 km²Andean
VargasLa Guaira298,1091,496 km²Capital
YaracuySan Felipe499,0497,100 km²Central - Occidental
ZuliaMaracaibo2,983,67963,100 km²Zulian
Dependencias Federales (maneo chini ya shirikisho)-2,245342 km²Insular (visiwa)
Distrito Federal Caracas (Mkoa wa shirikisho)-2,284,921433 km²Capital (mji mkuu)

Mgogoro wa kiuchumi

[hariri | hariri chanzo]

Mgogoro wa kiuchumi wa Venezuela ulianza mwongo 2010. Ulitokana kwa kiasi fulani na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani.[34] Sababu nyingine zilikuwa mfumko wa bei kali, ufisadi, usimamizi mbaya wa uchumi, na kutegemea kwa bidhaa moja, mafuta ya petroli. Kuporomoka kwa bei ya mafuta kulisababisha migogoro hii yote kutokea.[35]

Wakazi wengi (51.6%) wanajiainisha kama machotara wa Kizungu-Kiindio. Wazungu ni 43.6%, wenye asili ya Afrika ni 3.5% na Waindio 2.6%. Utafiti wa DNA unaonyesha kwamba urithi wa jeni kwa asilimia 60.6 ni wa Kizungu, 23 ni wa Kiindio na 16.3 ni wa Kiafrika.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania, ingawa lugha asilia zinakubalika kwa Waindio, na lugha nyingine zinatumiwa na wahamiaji.

Upande wa dini, 88% ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (71%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (17%).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Venezuela", The World Factbook (kwa Kiingereza), Central Intelligence Agency, 2025-12-26, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-31, iliwekwa mnamo 2026-01-05
  2. "UNSD - Welcome to UNSD". unstats.un.org. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  3. 1 2 "World Bank Open Data". World Bank Open Data. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  4. 1 2 "South America". MSN Encarta. Encarta. 13 Machi 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Aprili 2007. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  5. 1 2 "Annex tables" (PDF). World Urbanization Prospects: The 1999 Revision (kwa American English). Umoja wa Mataifa. 13 Machi 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 28 Agosti 2003. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  6. Van Cott, Donna Lee (2003). "Andean Indigenous Movements and Constitutional Transformation: Venezuela in Comparative Perspective". Latin American Perspectives (kwa American English). 30 (1): 49–69. ISSN 0094-582X kutoka JSTOR.
  7. "The Legacy of Hugo Chavez and a Failing Venezuela". Wharton Public Policy Initative (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Aprili 2019. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  8. David, Smilde (2025-12-21), "NACLA Report on the Americas", Wikipedia (kwa Kiingereza), juz. la 49, ku. 303–308, doi:10.1080/10714839.2017.1373956, ISSN 1071-4839, iliwekwa mnamo 2026-01-05
  9. "Venezuela Leads Region in Poverty Reduction in 2012, ECLAC Says". Center for Economic and Policy Research (kwa American English). 2013-12-06. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  10. "Venezuela Overview". Kundi la Benki ya Dunia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2018. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  11. Kevin Voigt (2013-03-06). "Chavez leaves Venezuelan economy more equal, less stable | CNN Business". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  12. "Venezuelans' Quality of Life Improved in UN Index Under Chavez", Bloomberg (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2026-01-05
  13. Juan Cristóbal Nagel (2026-01-07). "Poverty Shoots Up in Venezuela". Foreign Policy (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Machi 2018. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  14. "Venezuela: A Democratic Crisis". United States Department of State (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  15. "Standing with the Venezuelan People: One Year After Yet Another Sham Election". United States Department of State (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  16. 남민우, 기 (2018-05-02). "화폐경제 무너졌는데…최저임금 인상에 목매는 베네수엘라". 조선일보 (kwa Kikorea). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-12. Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  17. Trump says U.S. will 'run' Venezuela and sell seized oil in remarks on the strikes (kwa Kiingereza), NPR (Redio wa Umma wa Kimataifa wa Marekani), 2026-01-03, iliwekwa mnamo 2026-01-05
  18. "Trump anataka mafuta ya Venezuela, Je, mpango wake utafanikiwa?". BBC News Swahili. 2026-01-05. Iliwekwa mnamo 2026-01-09.
  19. Isidoro Losada, Ana María; Bitar Deeb, Rita (2022). "Introduction: Authoritarianism and Violence in Venezuela". Bulletin of Latin American Research (kwa Kiingereza). 41: 102–104. doi:10.1111/blar.13316.
  20. Human Rights Watch (2021-12-10), Venezuela: Events of 2021 (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2026-01-06
  21. "Statistical review of world energy" (PDF). BP (Mafuta ya Petroli ya Uingereza) (kwa Kiingereza). Juni 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-06-09. Iliwekwa mnamo 2026-01-06.
  22. "IMF sees Venezuela inflation at 10 million percent in 2019", IN (kwa Indian English), Reuters, 2018-10-09, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-26, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  23. Rosati, Andrew (2018-10-09), Venezuela's 2018 Inflation to Hit 1.37 Million Percent, IMF Says (kwa Kiingereza), Bloomberg.com, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-09, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  24. Gillespie, Patrick (2016-04-12), "Venezuela: the land of 500% inflation", CNNMoney (kwa Kiingereza), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-19, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  25. Gillespie, Patrick (2016-12-12), "Venezuela shuts border with Colombia as cash crisis escalates", CNNMoney, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-17, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  26. Rosati, Andrew (2017-01-11), "Venezuela's Economy Was the Worst Performing of 2016, IMF Estimates", Bloomberg.com, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-17, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  27. "Chamber of Commerce: 80% of Venezuelans are in poverty", El Universal (kwa Kiingereza), El Universal, 2016-04-01, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-04, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  28. Herrero, Ana Vanessa; Malkin, Elisabeth (2017-01-16), Venezuela Issues New Bank Notes Because of Hyperinflation (kwa Kiingereza), New York Times, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-20, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  29. Christophe Ventura (2025-02-01). "Venezuela's never-ending crisis". Le Monde diplomatique (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-06.
  30. "Venezuela situation | UNHCR" (kwa Kiingereza). UNHCR. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-21. Iliwekwa mnamo 2026-01-06.
  31. "Refugees and Migrants from Venezuela | R4V". Regional Inter-Agency Coordination Platform for Refugees and Migrants from Venezuela (R4V). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-26. Iliwekwa mnamo 2026-01-06.
  32. Gillespie, Patrick (2017-11-14), Venezuela just defaulted, moving deeper into crisis (kwa Kiingereza), CNNMoney, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-12, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  33. Venezuela in selective default, says credit ratings agency (kwa Kiingereza (Uingereza)), BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza), 2017-11-14, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-30, iliwekwa mnamo 2026-01-06
  34. Grant Castle (2024-01-23). "US Policy on Venezuela: A Road to Nowhere?". Chicago Policy Review (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-05.
  35. Sevil Omer (2025-06-24). "Venezuela crisis: Facts, FAQs, and how to help". World Vision (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-05.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela